Sijui jina yake,
Tumcall Mama Kavumbi.
Hapo kona ya kuenda mtaani,
Anauzanga tunjugu na mahindi choma.
I think nishaona ma pk hapo but siko sure.
Ye hukaa karibu na post ya stima.
Kabla hujamfikia kuna wamama wengine wawili,
But kuna vile Mama Kavumbi ako na kitu flani mysterious.
Sidhani ni mnormal.
Na si ati amechizi…
But ni kama alishagraduate hii maisha.
Mi huimagine ye si mhuman,
Amefikia kuwa being.
So kazi yake ni kuteremka huku…
Na kutuobserve.
Sioni ka hizo kavumbi ziuleta faida,
Ni kidogo kidogo tu.
Actually mi huona anaeza amua kula hio stock bila kushiba!
Akishawashanga kajiko pale na akasimamisha carton,
Apange stock, Akalie steni na atulie.
FYI napendaga mahindi choma,
Zake ziukaa zimeiva poa,
Ako na achari na ndimu haijachapa.
Shida ni moja… nimeshindwa kumwongelesha,
In fact naona ni madharau ata kujaribu.
Mtu kawaida kama mimi,
Nilete pang’ang’a za kavumbi… Siwesmek!
Hapa ni kazi na kukula kwa macho.
By the way hakuangi na wateja wengi,
So ni rare kupata mtu anaongea na yeye.
Kitu imenimess kichwa hapa,
Juzi Mtu wangu apite na gari.
Tumekaa ndani tukienda mrao,
Kuna mjengo hapo next so baro imejaa mawe,
Hii mtu iteremshe dirisha,
Iite Mama kavumbi amtolee mawe mbele,
Mama kavumbi aamke na atoe mawe,
Arudi atulie.
Mimi hapo nimetense,
Kwa nini anasumbua Mama Kavumbi?
Furthermore, haoni consciousness yake?
Hawako ligi koja na yeye!
Wacha miaka na hio taka taka yote,
Yaani hatambui Mama Kavumbi alishatranscend.
Inafaa tumsurround miguu tumskizie.
Tujue vile sisi pia tunaezagraduate,
Vile tunwezatulia tu.
Bila madistractions 1 million,
Hio level ya kuwa being ako that much closer to God.
Sijamuona for 2 weeks,
Sijui ako wapi na anaishi wapi,
Deep down na feel alimaliza kazi yake,
Amerudi pali alitoka ama ako mtaa ingine,
Bado akimaintain hio state ya kutulia.
In short natamani kutulia hivo,
I hope atarudi,
Nipate courage ya kumwaknowledge.
Hio tu!
Amarepoeta